MAADILI NA SERA
Ishi Nia Foundation tunaongozwa na dhamira ya kufuata viwango vya juu zaidi vya maadili. Kanuni yetu ya Maadili inahakikisha kuwa kila uamuzi na kitendo kinaendana na dhamira yetu ya kuinua na kuwezesha jamii. Sera zetu zinaakisi kujitolea kwetu kwa heshima, usawa, na uaminifu katika kila nyanja ya kazi yetu.
KANUNI ZETU ZA MAADILI
Uadilifu
Ishi Nia Foundation, tunaamini kuwa uadilifu ndio msingi wa kuaminika na uaminifu. Wanachama wetu wamejitolea kutenda kwa uaminifu, heshima, na haki katika kila mahusiano.
Tunalenga kuwa mfano wa kuigwa kwa kuhakikisha kuwa matendo yetu yanaendana na dhamira na maadili yetu. Kwa kukuza utamaduni wa uadilifu, tunalenga kuhamasisha imani na kujenga uhusiano wa kudumu na wale tunaoshirikiana nao.
Wajibu
Jukumu letu Ishi Nia Foundation ni kuwa kichocheo cha mabadiliko chanya. Tunatanguliza ustawi wa jamii na kuhakikisha kuwa kila uamuzi na kitendo hufanywa kwa maslahi ya wale tunaowahudumia.
Tunakubali wajibu wetu wa kuinua na kuwezesha, tukitengeneza mazingira ambayo kila mtu anaweza kustawi. Kwa kutenda kwa makusudi na kujitolea, tumejizatiti kuleta mabadiliko yenye maana katika maisha ya watu walioko katika mazingira magumu.
Utofauti na Ujumuishi
Utofauti na ujumuishaji ni misingi muhimu ya dhamira yetu. Tumejitoa kuunda mazingira ambapo kila mtu anahisi kuthaminiwa na kuheshimiwa, bila kujali asili yake, jinsia, umri, au uwezo wake.
Kwa kukumbatia ujumuishaji, tunaimarisha uwezo wetu wa kutatua changamoto ngumu na kuchochea ubunifu. Tunaamini kwamba maendeleo ya kweli yanawezekana tu pale kila mtu anapopewa nafasi ya kushiriki na mchango wake kutambuliwa.
Uwajibikaji na Uwazi
Uwajibikaji na uwazi ni kiini cha namna tunavyofanya kazi. Tunazingatia kwa umakini sheria na kanuni zinazotoa mwongozo kwa mashirika yasiyo ya kiserikali, kuhakikisha kuwa kila hatua na uamuzi vinaendana na maslahi ya umma.
Tunatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu jinsi rasilimali zinavyogawiwa na kusimamiwa, tukisisitiza matumizi bora na yenye ufanisi. Kwa kushikilia misingi hii, tunajenga uaminifu, kuimarisha uhalali wetu, na kuonesha kujitolea kwetu kwa maadili na uwajibikaji.
SERA ZETU
Sera ya Kupinga Unyanyasaji
Tumejizatiti kuhakikisha mazingira ya kazi yasiyo na unyanyasaji, ambapo kila mtu anahisi kuheshimiwa, kuthaminiwa, na kuungwa mkono. Unyanyasaji wa aina yoyote iwe wa maneno, kimwili, au wa kisaikolojia unaofanywa na au kuelekezwa kwa mtu yeyote anayehusiana na Taasisi unakatazwa kabisa.
Sera ya Kupinga Ubaguzi
Tunahakikisha fursa sawa na heshima kwa wote, bila kujali rangi, kabila, dini, jinsia, utambulisho wa kijinsia, mwelekeo wa kijinsia, asili ya taifa, umri, ulemavu, hali ya ndoa, au sifa nyingine yoyote inayolindwa kisheria. Kila mtu anathaminiwa kwa mchango wake wa kipekee.
Sera ya Usiri
Heshima na usiri ni misingi ya kazi yetu.
Taasisii inachukua kila tahadhari kulinda taarifa nyeti zinazokabidhiwa kwetu, kuhakikisha zinashughulikiwa kwa uangalifu na taaluma. Kanuni kuu ni pamoja na
- Kwa Ujumla: Taarifa zinazokusanywa na Taasisi hazitatumika kwa manufaa binafsi kwa namna yoyote ile.
- Wafadhili: Usiri na kutotambulika kwa wafadhili vinalindwa kwa umakini mkubwa, na upatikanaji wa taarifa zao umedhibitiwa vikali.
- Wapokeaji wa Ruzuku: Usiri wa taarifa nyeti kutoka kwa mashirika na taasisi zinazopokea ruzuku unahifadhiwa wakati wote.
- Mikataba na Ruzuku: Maelezo ya miamala na mashirika ya kitaaluma au biashara yanashughulikiwa kwa kiwango cha juu kabisa cha usiri.
- Mikutano: Majadiliano, maamuzi, na maoni yanayotolewa katika mikutano ya Bodi na kamati hushughulikiwa kwa usiri mkali.
Sera ya Kufuta Taarifa
Sera ya Kufuta Taarifa inaeleza jinsi watumiaji wanavyoweza kuomba kufutwa kwa taarifa zao zilizokusanywa kupitia huduma zetu, ikiwa ni pamoja na zana zozote zilizounganishwa na Facebook, Instagram, au majukwaa mengine.
Ikiwa ungependa taarifa zako zifutwe kutoka kwenye mifumo yetu, tafadhali tumia fomu ya mawasiliano.
Mara tu tutakapopokea ombi lako, tutafanya yafuatayo: Kuthibitisha utambulisho wako (ikihitajika), Kufuta taarifa zako binafsi kutoka kwenye mifumo yetu, na Kutuma barua pepe ya uthibitisho ndani ya siku 7 za kazi.
Katika baadhi ya matukio, tunaweza kuhitajika kisheria kuhifadhi taarifa fulani kwa muda maalum (kwa mfano, kwa ajili ya kufuata masharti ya sheria au kuhifadhi kumbukumbu). Katika hali hizi, taarifa zako zitahifadhiwa kwa usalama hadi pale zitakapoweza kufutwa kabisa.





